MFUKO WA GEPF WATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) KATIKA SHULE YA MSINGI YA MATUMAINI YA JESHI LA WOKOVU ILIYOPO KURASINI

Meneja Masoko wa Mfuko wa GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina akiongea na vyombo vya habari juu ya mipango ya Mfuko huo kutoa misaada kwa jamii hasa kwa wale wenye mahitaji kama walemavu wa ngozi (Albino)


 Mtoto Maria Mwingira akipokea msaada wa mafuta maalum ambayo hukinga ngozi yao wakati wa jua kali kutoka kwa Meneja Masoko wa GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina.…
Kijana Salum Iddi akitoa neno la shukurani kwa Mfuko wa GEPF kwa niaba ya watoto wenzake huku akisikilizwa kwa makini na Meneja Masoko wa GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina pamoja na Afisa Uendeshaji wa Mfuko huo,Bi. Zuwena Rajabu.

Afisa kutoka GEPF,Bw. Gaudence Mkoba akikabidhi misaada hiyo kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Matumaini.

Mkurugenzi wa Shule ya Msingi ya Matumaini Bw. Chacha akizungumza na baadhi ya watoto wa shule hiyo huku mwenyekiti wa umoja wa Albino wilaya ya Ilala Bw Seif Ulate akifuatilia kwa makini.

No comments

Powered by Blogger.