MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KUFANYIKA KITAIFA MKOANI NJOMBE


 Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt. Fatma Mrisho akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani isemayo, Tanzania Bila Maambukizi Mapya ya VVU, Vifo vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi na Unyanyapaa inawezekana inayolenga kupunguza maambukizi Mapya ya Ukimwi, kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na kukomesha vitendo vya unyanyapaa kwa asilimia Sifuri.…
 Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani yatakayofanyika kitaifa mkoani Njombe kuanzia Novemba 24, 2014 na kufikia kilele chake Desemba 1, 2014.

 Mkurugenzi wa ufuatiliaji wa Tathmini wa Ofisi ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi  Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu utoaji wa huduma na upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa watu wanaoishi na VVU katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa TACAIDS akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mbinu na elimu inayotolewa na TACAIDS katika maeneo mbalimbali ikiwemo matumizi ya mipira ya kike kwa wanawake ili kuzuia maambukizi mapya ya VVU.

No comments

Powered by Blogger.