JUMLA YA WASICHANA 6,000 MKOANI MTWARA WAPO KATIKA NAFASI NZURI YA KUJIKINGA NA MIMBA NA VIRUSI VYA UKIMWI‏

Baadhi ya wanafunzi wa kike wakipata semina kutoka  T-MARC kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Wanafunzi wa kike wakiwa wenye furaha baada ya semina T-MARC kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Na hawa ni wanafunzi wengine waliopata mafunzo kutoka  T-MARC kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).


Na Mwandsihi Wetu
Jumla ya wasichana 6,000 mkoani Mtwara walio kwenye umri wa balehe sasa wapo katika nafasi nzuri ya kujikinga na mimba za umri mdogo zinazowasababishia kuacha shule pamoja na kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi             
Akiongea na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Meneja uhusiano na mawasiliano wa T-MARC Tanzania Maurice Chirimi alisema mafanikio hayo yametokana na mradi unaojulikiana kama ‘Hakuna Wasichoweza’ unaotekelezwa na T-MARC kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.
Chirimi alisema kuwa, mradi huo ulianza mwaka 2013 ambapo USAID kwa kushirikiana na Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii (Vodacom Foundation waliwapa nguvu ili kufanikisha mradi huo.
Alifafanua kuwa, kupitia mradi huo, T-MARC imefanikisha kutoa mafunzo kwa wasichana walio mashuleni na wasio mashuleni ikiwa na lenga la kuwapatia elimu pamoja na kuwapatia pedi wasichana wanatoka katika familia maskini kwa ajili ya kujihifadhi wakati wakiwa hedhi.
Aliongeza kuwa, mafunzo pamoja na pedi za bure zimewafikia wasichana 5,232 waliopo katika shule 24 za msingi na wengine 552 wasiokuwepo mashuleni katika kata 17 mkoani Mtwara.
“Mafunzo ya namna na kujihifadhi wakati wakiwa hedhi pamoja na afya ya uzazi yanafanyika chini ya uwezeshaji wa walimu waliopewa mafunzo na wauguzi wa jadi. Kitini cha kufundishia juu ya masuala haya kimeweza kuandaliwa na T-MARC kwa kushirikiana Taasisi ya Elimu Tanzania kupitia mradi huu wa ‘Hakuna Wasichoweza’,” alifafanua
Alisema kupitia mafanikio yaliyopatikana kwenye awamu ya kwanza ya mradi, T-MARC kwa msaada wa dola za Kimarekani 166,000 itaupanua mradi na kuwafikia wasichana wengine 4,200 katika shule mpya 10 na kuongeza kuwa pia shirika lake litawapatia mafunzo walimu wengine 20 kwa ajili ya kuwafundisha na kuwaelekeza wasichana
Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia alisema Vodacom Foundation ikitambua mchango wa mwanamke katika jamii inayomzunguka kwani ukimwelimisha mwanamke ni sawasawa na kuelimisha jamii, Kwa kweli Vodacom foundation inajivunia sana kufadhili mradi huo muhimu.
Alisema mara nyingi ukosefu wa elimu sahihi juu ya afya ya uzazi umekuwa ukiwafanya wasichana kuanza kuacha kuhudhuria vipindi vyao mashuleni yote hayo pia ni kwa kukosa nguo za kujihifadhi wakiwa katika siku za hedhi na kuwafanya watoto kuanza ngono wakiwa katika umri mdogo bila kujua madhara yake jambo ambalo huwasababishia mimba na kuwafanya washindwe kutimiza ndoto zao za kielimu

No comments

Powered by Blogger.