WANANCHI GEITA WATUMIA VITAMBULISHO VYA TAIFA VYA WENZAO BAADA YA KUKOSA FURSA YA KUVIPATA NIDA
Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini.Joseph Musukuma akizungumza na Wananchi wa Kata za Nzera na Rwezera wilayani Geita katika mkutano wa hadhara alioufanya jana mkoani humo.
Na Victor Bariety, Geita
BAADHI ya Wananchi wa Kata za Nzera na Rwezera wilayani Geita wamesema wanalazimika kusajili line kwa kutumia vitambulisho vya Taifa vya watu wengine kwa kuwa zoezi la uandikishaji liliwapita kushoto na kuiomba serikali iangalie uwezekano wa kurudia zoezi hilo ila wasije wakakumbana na mkono wa sheria.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, kwenye mikutano ya hadhara ya Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini.Joseph Musukuma,iliyofanyika kwenye kata hizo wananchi hao wamesema wakati wa zoezi hilo maeneo mengi ya jimbo lao hayakufikiwa jambo ambalo limewasababishia usumbufu mkubwa hasa wanapohitaji huduma inayohusiana na kitambulisho cha NIDA.
Akijibu kero hiyo,mbunge musukuma amemuomba GHULAM kufikisha kero hiyo kwa Rais wa Tanzania Samoa Suluhu Hassan na ikimpendeza zoezi hilo lirudiwe.
"Mheshimiwa mbunge,suala la NIDA linatutesa sana wananchi,tunalazimika kusajili line kwa kutumia NIDA za watu,tunajua ni kosa lakini tutafanyaje,serikali itusaidie zoezi hili litufikie wananchi wa vijijini," alisema Mashaka Masele huku akishangiliwa.
Mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya soko kuu la Nzera, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali, akiwepo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (MNEC) Mkoa wa Geita , Nadra Ghulam kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda.
Kwa upande wake mjumbe huyo wa NEC mbali na kuahidi kufikisha kilio hicho panapohusika,aliwataka wananchi kuwa na imani na serikali yao.
"Mheshimiwa mgeni rasmi,umewasikia wananchi,hili zoezi la NIDA ni kero kubwa,wakati wa uandikishaji,wananchi hawakujua umuhimu wake lakini kwa sasa kila wanakoenda wanatakiwa wawe na NIDA ndio maana wameanza kuona umuhimu wake nikuombe kamwambie mama yetu Rais Samia ikimpendeza hili zoezi lirudiwe upya,wananchi wanapata usumbufu mkubwa kwa kukosa NIDA"alisema Musukuma huku akishangiliwa na wapiga kura wake.
"Ndugu wananchi niwaombe tu,tuwe na imani na viongozi wetu na tuwasifie pale wanapofanya vizuri,sio tusubiri mpaka waondoke ndio tuwasifie, "alisema Ghulam.
Post a Comment