HALMASHAURI MANYONI YATOA MIKOPO YA MIL.108/-, MWENGE UHURU WAZINDUA MIRADI

 

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota, akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru 2023 baada ya kukabidhiwa ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kuanza mbio zake wilani humo kwa ajili ya kutembelea, kuweka jiwe la msingi na kukagua miradi ya maendeleo Septemba 28, 2023. 

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota, akimkabidhi Risala ya Utii Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim ili akamkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan.

Viongozi wa Wilaya ya Manyoni wakiwa katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru baada ya kumaliza mbio zake wilayani Itigi. 

Thobias Mwanakatwe, MANYONI

HALMASHAURI ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida imefanikiwa kutoa mikopo ya Sh.milioni 108 ambayo ni sawa na asilimia 48 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu hadi kufikia Juni mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni,Kemirembe Lwota, katika risara yake jana ya utii kwa rais Dk.Samia Suluhu Hassan wakati kuhitimisha mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo,alisema mikopo hiyo ni kati ya Sh.milioni 224.4 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kutoa mikopo katika mwaka wa fedha 2022/2023.

Lwota alisema Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni umetembelea na kukagua miradi yenye thamani ya Sh.bilioni 1.236 ambayo ni ujenzi wa barabara ya Manyoni-Msigati yenye urefu wa mita 700 kwa kiwango cha lami nyepesi kwa gharama ya Sh.milioni 589.

Mingine ni mradi wa uhifadhi  wa chanzo cha maji Kaloleni ambao unahudumia wakazi 5,271 waliopo katika mitaa ya Ujasiriamali,Mwanzi,Mitoo ya Chini,Kaloleni na Samaria, kiwanda cha kisasa cha kubangua korosho kilichojengwa katika kijiji cha Ilucha kilichojengwa kwa Sh.milioni 568,Zahanati ya kijiji cha Mbwasa iliyojengwa kwa Sh. milioni 77.6 ambayo itahuhudumia wakazi 2,526.

Miradi mingine iliyotembelewa na Mwengenwa Uhuru ni ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya elimu ya awali katik kinijicha  Chikuyu yaliyojengwa kwa Sh.milioni 64.9 kikundi cha vijana cha Imani - Majiru ambao wamenunua pikipiki ya magurudumu matatu na mradi wa madawati 300 yaliyonunuliwa kwa halmashuri ya Wilya ya Manyoni kwa fedha za ndani Sh.milioni 21.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023,Abdalla Shaibu Kaim, akizungumza baada ya kutembelea mradi wa maji Kaloleni, aliwataka wananchi kulinda vyanzo vya maji kwa kutofanya shughuli za kilimo na ufugaji ndani ya vyanzo hivyo.

Alisema ipo wazi kuwa hairuhusiwi kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya vyanzo vya maji mita 60 na kuwagiza viongozi wa wilaya hiyo kuimarisha ulinzi ili visiharibiwe.

No comments

Powered by Blogger.