Waziri Mbarawa aridhishwana kasi ya ujenzi TBIII
Mkurugenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Wolfgang Marschick (kushoto) akiwa na Mhe. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akikagua mradi wa jengo hilo.
Meneja wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Ray Blumrida (wa pili kulia) akielezea ujenzi wa ngazi zinazotumia umeme (escalator) kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo leo.
Mhe. Prof. Makame Mbarawa mwenye miwani mkononi, akiendelea leo na ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Kushoto ni Mkurugenzi wa mradi huo Bw. Wolfgang Marschick na kulia ni Meneja wa Mradi Bw. Ray Blumrida.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa (katikati), akimsikiliza Meneja wa mradi wa ujenzi la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Ray Blumrida akielezea ujenzi wa madaraja (bridges) ya kupitia abiria wanaowasili na wanaoondoka.
Na Neema Harrison, TUDARCO
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa
ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ambapo sasa utakamilika Oktoba 2018.
Mhe. Prof. Mbarawa aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea
maendeleo ya mradi huo ulianza 2013, na sasa kuridhishwa na hatua waliyofikia.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo, Prof. Waziri Prof. Mbarawa
amesema kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 64, na hatua iliyobaki ni ujenzi wa wa
mifumo ya ndani ya jengo.
“Sote tumekuwa mashahidi nimekuwa nuikitembelea mara kwa mara ujenzi wa
jengo hili na ninaridhika kwa kasi ya ujenzi wake, ambapo sasa tumefikia kwenye
hatua nzuri na vitu vilivyobaki sio vikubwa kama ilivyokuwa wakati wanaanza,
hivyo ni matumaini yangu hadi Oktoba mwakani (2018) jengo lote litakuwa
limekamilika na serikali kukabidhiwa,” amesema Mhe. Prof. Mbarawa.
Hatahivyo, Prof.
Mbarawa amesema serikali inatarajia kupata watalii wengi na
serikali itapata mapato kupitia kodi na tozo za abiria wanaosafiri kutumia kiwanja
hiki, pia wapangaji wanaotoa huduma mbalimbali yakiwemo maduka na usafiri wa
magari.
Amesema serikali itaendelea kutoa fedha za ujenzi wa jengo hilo linalosimamiwa
na mkandarasi BAM International ya Uholanzi, ambapo pia likikamilika litatoa
ajira kwa Watanzania wengi.
“BAM wamekuwa wakifanya kazi nzuri nawapongeza sana na tunatarajia hadi
kukamilika tutapata mradi bora utakaoliingizia taifa faida kubwa kutokana na kodi
na tozo mbalimbali,” amesema Prof. Mbarawa.
Amesema jengo hilo likikamilika linatarajia kuchukua abiria milioni sita (6) kwa
mwaka, na kupunguza msongamo ulipo katika jengo la pili la abiria (JNIA-TBII)
Post a Comment