NEYMAR ATUA MAZOEZINI BARCELONA KWENDA KUAGA

Staa wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar amepewa ruhusa ya kwenda kumalizia mambo yake muda mfupi baada ya kuwasili katika mazoezi ya klabu yake ya Barcelona, leo asubuhi.
Neymar ambaye alikuwa nchini China kwa ajili ya masuala ya kibiashara, aliwasili katika mazoezi ya hayo lakini alidumu kwa dakika 43 bila kufanya mazoezi kisha akaondoka.
Inadaiwa kuwa alipewa ruhusa na kocha wake kwenda kumalizia masuala yake ya usajili wa kutua Paris Saint-Germain kwa ada ya pauni milioni 196.
Radio ya RAC1 ya Hispania imeripoti kuwa Neymar alifika mazoezini hapo kuagana na wenzake kabla ya kukamilisha dili la kuhamia PSG. 

No comments

Powered by Blogger.