Msemaji wa Jeshi la Kenya ajitokeza
- Wizara ya Ulinzi nchini Kenya imekanusha taarifa zilizosambazwa kwamba Msemaji wa Jeshi la Kenya Kanali Joseph Owuoth alikuwa ametoweka.Waziri wa Ulinzi Bi. Raychelle Omamo, amesema, taarifa kama hizo zinatishia usalama na kuzua wasiwasi miongoni mwa maafisa wa jeshi na familia zao.
- Kanali Owuoth aligonga vichwa vya habari baada ya kuthibitisha kwamba nyaraka zilizokuwa zimetumiwa na muungano wa upinzani nchini humo NASA kudai kwamba serikali inapanga kutumia jeshi kutekeleza 'mapinduzi' ili kuendelea kusalia madarakani zilikuwa halisi.
- Hata hivyo, Msemaji huyo alisema nyaraka hizo zilinukuliwa na kufasiriwa visivyo.
- Bi Omamo, kwenye kikao hicho, alisema baada ya uchunguzi, imebainika kwamba nyaraka hizo zilizotumiwa na muungano wa NASA zilikuwa za kughushi.
- Taarifa za kudaiwa kutoweka kwa Kanali Owuoth zilikuwa zimezua wasiwasi mkubwa kwani zimetokea siku moja baada ya mwili wa Meneja wa Tehama katika Tume ya Uchaguzi Kenya, Chris Msando, aliyetoweka Ijumaa usiku, na kukutwa ameuwawa katika eneo la Kikuyu nje ya viunga vya jiji la Nairobi .
Post a Comment