Wanaharakati Wamkalia kooni mke wa Mugabe
Shirika la wanaharakati nchini Afrika Kusini, LA Afriforum, leo limetangaza nia yake ya kuwasilisha maombi yake mbele ya Mahakama ya kutaka mke wa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aondolewe kinga ya kidiplomasia iliyotolewa na serikali ya Afrika Kusini
Grace Mugabe anatuhumiwa kumshambulia binti mmoja ,Gabriella Engels, jijini Johannesburg, takriban wiki mbili zilizopita.
Kiongozi wa Afriforum, Kallie Kriel, amesema, kumpa mkewe Rais Mugabe kinga ya kidiplomasia ni kinyume cha sheria kwa sababu, kinga ya kidiplomasia haiwezi kutumika katika kesi kubwa ya uhalifu na unyanyasaji kwa mujibu wa sheria za Afrika Kusini.
Grace Mugabe alirejea Zimbabwe jana Jumapili licha ya kutafutwa na polisi wa Afrika Kusini.
Mawakili wa Gabriella Engels mwanamke ambaye anamtuhumu Bi Mugabe kwa kumshambulia wamesema, mteja wao alipewa pesa kuachana na kesi hiyo lakini akakataa.
Post a Comment