RAHEEM STERLING AIOKOA MAN CITY YATOKA 1-1


Raheem Sterling ameiokoa Manchester City iliyobakia na wachezaji 10 na kuinyima Everton ushindi katika usiku ambao Wayne Rooney alifunga goli lake la 200 la Ligi Kuu ya Uingereza. Manchester City walijikuta na kibarua kigumu baada ya Rooney kufunga goli na baada ya Kyle Walker kutolewa nje kwa kadi mbili za njano za haraka ndani ya dakika 44.
Kikosi hicho kinachonolewa na Pep Guardiola hakikuamini matokeo hayo na kilipambana mnono na kufanikiwa kuepuka kipigo cha pili nyumbani wakiwa chini ya Mhispania huyo.
 Mpira uliopigwa na Wayne Rooney ukiwa umempita tobo kipa wa Manchester City na kuandika goli 
 Raheem Sterling akiachia shuti na kuisawazishia Manchester City goli na kufanya matokeo kuwa 1-1

No comments

Powered by Blogger.