MADIWANI UKAWA WADAI MAKONDA ANAWADHARAU


                                                    
                        Meya wa manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob

Dar es Salaam. Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob amedai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekuwa na tabia ya kudharau na kutoheshimu viongozi wenzake, hasa wa upinzani akiwaona hawatendi kazi vizuri.akijibu tuhuma hizo jana, Makonda amesema: “Huyo anayelalamika mwambie huo anaoufanya ni utoto akikua ataacha. Narudia tena siyo kazi yangu kuangalia nani hajaja kwenye kikao.”Kauli hiyo ya Jacob kwa niaba ya wenzake, imekuja baada ya madiwani wa Ukawa wa Manispaa ya Kinondoni kususa kikao kilichoitishwa na Makonda.Makonda aliitisha kikao cha wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara za manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni na madiwani wote, wakiwamo wabunge wanaounda halmashauri hizo.Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Arnaoutoglou kililenga kuzungumzia masuala mbalimbali, kama maeneo yaliyovamiwa na uboreshaji wa elimu mkoani Dar es Salaam.

(chanzo mwananchi)
 

No comments

Powered by Blogger.