HAMKANI SI SHWARI SUDAN KUSINI
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu kuwepo kwa hali
mbaya ya kibinaadam nchini Sudan kusini , maelfu ya watu wakiyakimbia makazi
yao kutokana na machafuko.Shirika la kuhudumia wakimbizi linasema Njaa na
maradhi vinatishia maisha ya maelfu ya watu ambao wamebaki nchini humo.
Makundi ya watu wenye silaha pia yamewazuia watu wengi
kuingia nchi jirani ya Uganda na kuna ripoti ya kuwepo na vitendo vya watoto
kusajiliwa kwa nguvu kwenye jeshi.Upungufu mkubwa wa chakula na mlipuko wa
maradhi ya kipindupindu umefanya hali kuwa mbaya zaidi.
Mpango wa kumaliza mapigano kati ya Serikali ya Rais Salva
Kiir na mpinzani wake mkubwa Riek Machar ulivunjika mwezi uliopita.Katibu mkuu
wa masuala ya kibinaadam wa umoja wa Mataifa, Stephen Obrien amesema mahitaji
ya Sudani kusini ni Changamoto kubwa ''tunaweza kushuhudia , watu wengi wengi
wanahitaji huduma, wanahitaji kusaidiwa, lakini zaidi wahitaji kulindwa.
Hivyo tunahitaji si tu kutazama maeneo yanayozunguka kambi
hapa, lakini tunapaswa kutazama nje pia na kufikiria namna gani wau hawa
watalindwa dhidi ya machafuko. Hasa wanaoathirika ni watoto na wanawake,
wagonjwa na walemavu wanaohitaji msaada, hiyo ni changamoto kubwa tunayopaswa
kuikabili''
chanzo bbc.
Post a Comment