MO DEWJI AANZA FUJO SIMBA, AMWAGA MILIONI 100 ZA USAJILI

Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji akimkabidhi Rais wa Simba, Evans Aveva mfano wa hundi ya Sh. Milioni 100 leo mjini Dar es Salaam.
 Mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Mohamed Dewji ''Mo'', leo hii ameikabidhi klabu ya Simba kitita cha shilingi milioni 100 kama mchango wake kwa ajili ya kuisaidia klabu hiyo katika zoezi zima la usajili. Simba ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa fedha ili iweze kukamilisha usajili wake kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kuanza kutimua vumbi, Agosti 20 mwaka huu. Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo Rais wa Simba, Evans Aveva amesema kuwa kiasi hicho kitasaidia kupunguza mzigo mkubwa walio kuwa wameubeba ili kukamilisha zoezi hilo la usajili.Mpaka kufikia sasa tulikuwa tunadaiwa shilingi milioni 420 ili kukamilisha usajili wetu, lakini kwa kiasi hiki cha fedha ambazo Mo ametupatia kimetusogeza na tumebakiza milioni 320 ili kukamilisha zoezi hilo.Tunawaomba wanachama wetu wengine ambao wataguswa na hali hiyo waweze kutusaidia kama alivyofanya Mo.

No comments

Powered by Blogger.