MENEJA WA DIAMOND PLATNUMZ, BABU TALE AKAMATWA NA POLISI LEO ASUBUHI
Meneja
wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu
kwa jina la ‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi mwa polisi Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam.
Babu
Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa
nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru
alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.
Babu
Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake
na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila
ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.
Post a Comment