KIPA JOE HART AGEUKA SHUJAA BAADA YA KUIWEKEA NGUMU SLOVENIA

 Uingereza inapaswa kushukuru umahiri wa kulinda goli wa kipa Joe Hart na kuwa na bahati kwa kiasi fulani baada ya kuambulia sare tasa dhidi ya Slovenia, katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia 2018.

Hart ambaye anachezea kwa mkopo Torino, ambaye alionekana kama asiyehitajika Manchester City, amemuokoa na aibu kocha wa muda Gareth Southgate ya kupoteza mchezo wa jana kwa timu ambayo ni ya 67 katika viwango vya soka duniani.

Hart alimnyima magoli Josip Ilicic baada ya kupigiwa pasi mbovu na Eric Dier na Jordan Henderson, lakini kali zaidi aliyotoa kipa huyo ni pale alipopangua mpira wa kichwa wa Jasmin Kurtic na kuutoa nje katika kipindi cha pili.
       Kipa Joe Hart akiruka juu na kupangua mpira kwa mkono wa kushoto
 Kipa Joe Hart akianguka chini baada ya kupangua mpira na kuutoa nje
   Homa ya mchezo ilipanda kiasi cha kujikuta wachezaji wakitaka kuzichapa

No comments

Powered by Blogger.