Tume ya Uchaguzi yavitaka Vyombo vya Habari nchini kuiga wenzao wa Kenya
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani (kulia) akifafanua jambo wakati akizungumza na Mtangazaji wa Azam Tv, Nurdin Selemani kupitia kipindi cha Mizani ya Wiki kilichorushwa jana Jumapili hii.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani
(kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando baada ya kushirikia kwenye kipindi cha Mizani ya Wiki kinachorushwa na Azam Tv Jumapili usiku.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani (kushoto) ,akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi huo.Picha na Hussein Makame.
Na Mwandishi Maalum
MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima
Ramadhan amevitaka vyombo vya Habari vya Tanzania viige mfano wa wenzao
wa Kenya kwa kutumia muda mwingi kutoa Elimu ya Kupiga kura.
Akizungumza kwenye kipindi cha Mizani ya Wiki kinachorushwa na Kituo cha
Televisheni cha AZAM Jumapili usiku, Ramadhan alisema moja ya mambo
aliyojifunza katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya ni jinsi vyombo vya Habari
vilivyoshiriki katika Uchaguzi huo na kuchangia watu wengi kujitokeza kupiga
kura..
“Natamani na sisi vyombo vya hapa nyumbani viige wenzao wa Kenya ambao
walitoa muda mwingi kwa kutoa Elimu ya Mpiga kura,” alisema Ramadhani. aliongeza kuwa baadhi ya mambo ambayo amejifunza kwa
Tume Huru na Mipaka ya Kenya (IEBC) katika uchaguzi mkuu uliomalizika hivi
karibuni ni usambazaji wa vifaa katika vituo vya kupigia kura.
Alifafanua kuwa licha ya kuwa Kenya wana vituo vichache takribani 40,000 vya
kupigia kura ukilinganisha na vya Tanzania ambako kuna vituo 65,000, lakini
alisema walifanya vizuri kwenye kusambaza vifaa.
Eneo lingiine ambalo lilimvutia ni namna wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi
katika Kituo cha kupigia kura wanavyokuwa na uelewa mkubwa kuhusu
taratibu za kupiga kura.
Kuhusu kuruhusu wafungwa na Wakenya walioko nje kupiga kura, Kailima alisema kwa sasa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi hairuhusu jambo hilo
na akaongeza kuwa Tume haina pingamizi iwapo wabunge watatunga sheria
inayoruhusu makundi hayo kujiandikisha na baadaye kupiga kura.
“Tume ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuamua ni nani apige kura, ila
tunaongozwa na katiba pamoja na sheria,” alisema.
Akizungumza utaratibu wa kupiga kura uliotumika Kenya, alisema ni mzuri lakini akaongeza kuwa utaratibu unaotumiwa na NEC uko wazi
ukilinganisha na ule uliotumiwa na IEBC.
“Utaratibu wetu ni mzuri zaidi kwani unatoa fursa ya mawakala kujiridhisha
kwamba mtu aliyeenda kupiga kura ndiye mwenyewe, unapunguza kelele,”
alisema .
Akilinganisha teknolojia iliyotumiwa na IEBC, Ramadhan alisema inawezeshwa
mtu akipiga kura inahesabiwa jambo ambalo ilisababisha IEBC kutangaza
matokeo ya awali ambayo hayajathibitishwa na akaongeza kuwa hilo ni jambo
la hatari kwa kuwa matokeo ya pili yakibadilisha matokeo ya awali inaweza
kuleta sintofahamu.
Alisisitiza kwamba mfumo ambao unatumiwa na NEC bado pia ni mzuri kwa
kuwa unalenga kutangaza matokeo ambayo yameshathibitishwa na yanaleta
amani kwa jamii.
“Uchaguzi ulipita tulitangaza matokeo ya urais ndani ya saa 72 kwa hiyo
tuliwahi kuliko wenzetu wa Kenya.”

Post a Comment