TFF YAFUNGUKA KITENDO CHA HAJI MANARA KUPOKEA VIFAA VYA YANGA

Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limezungumzia juu ya kitendo cha Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara kuiwakilisha Klabu ya Yanga katika shughuli ya kukabidhi vifaa vya msimu wa 2017/18.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa juzi na Kampuni ya Vodacom ambao ni wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo Yanga hawakupeleka mwakilishi wao katika shughuli hiyo, ndipo Manara akajitokeza jukwaani na kusimama na wanamitindo waliokuwa wakionyesha jezi mpya za Yanga.
Kitendo hicho kimepokelewa kwa hisia tofauti hasa na mashabiki wa Yanga ambao wameonyesha kutofurahishwa na tukio hilo.
Akizungumzia suala hilo, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema: “Haji alifanya vile kwa kuwa wale ni watani wa jadi, kuna watu wanatafsiri Yanga na Simba ni wapinzani wa jadi, hao ni wa watani wa jadi. Haji Manara alifanya vile akiwa katika mazingira ya kufanya vile ili amsaidie mtani wake.”

No comments

Powered by Blogger.