Kagame ashinda Tena Urais
Rais wa Rwanda, Paul Kagame ameshinda uchaguzi nchini Rwanda kwa asilimia 98 ya kura zote zilipopigwa hivyo ataongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu mfululizo.
Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda imesema kuwa kiongozi huyo ameshinda kwa asilimia 98 na kuwabuluza wapinzania wake Frank Habineza na Philippe Mpayimana ambao walikuwa wakigombea nafasi hiyo.
Baaada ya ushindi huu, Kagame ataongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu wa miaka saba na anaweza kuongoza tena kwa muhula wa nne wa miaka saba mpaka mwaka 2034 kwa mujibu wa Katiba ya Rwanda.
Rais wa Rwanda Paul Kagame aliingia madarakani tarehe 24 Machi mwaka 2000
Post a Comment