Kufuatia kujitokeza kwa makosa ambayo yalichangia Yanga kukosa sherhe za kukabidhi vifaa vya udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeomba radhi kwa kilichotokea.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kilichotokea ni kosa ambalo lilisababishwa na Bodi ya Ligi katika kuwatumia Yanga taarifa juu ya kuhuduria mchakato huo, hivyo kwa kuwa Bodi ya Ligi ipo chini yao, wao TFF wanaomba radhi kwa kilichotokea.
Lucas amesema kuwa kulifanyika mawasiliano jioni ya juzi Jumatano, hivyo inavyoonekana Yanga hawakupata taarifa hiyo na ndiyo maana hawakuhudhuria.
Katika taarifa yao waliyoitoa leo asubuhi, Yanga walisema wamesikitishwa na suala hilo na kuagiza waombwe radhi kwa maandishi.
Akizungumzia hilo, Alfred Lucas alisema kwa kuwa Yanga wamelalamika kwa mdomo, nao wamewaomba radhi kwa mdomo, wakiomba kwa maandishi nao watawajibu hivyohivyo.
Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura naye alizungumzia suala hilo kwa kusema kuwa wanaomba radhi kwa kilichotokea kwa kuwa hilo ni kosa lao.
Post a Comment