MKATA UMEME WA YANGA AFUNGASHIWA VIRAGO VYAKE

Klabu ya Yanga kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Boniface Mkwasa imethibitisha kuwa wameachana na kiungo mkabaji Justine Zulu maarufu kwa jina la Mkata Umeme.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa msimu uliopita wakati wa dirisha dogo la usajili Disemba, 2016 hakuonyesha kiwango kizuri na pia aliandamwa na majeraha katika msimu huo uliopita.
“Zulu alisajiliwa na Yanga mkataba wake ulikuwa mwaka mmoja na bila kuficha kiwango chake hakikuwa cha kutridhisha, hivyo klabu imeamua kumpa nafasi mtu mwingine,” alisema Mkwasa.
Ameongeza kuwa wameshakubaliana na mchezaji huyo kupitia kwa wakala wake juu ya kufidia muda wa mkataba wake uliosalia.

No comments

Powered by Blogger.