POLISI KENYA WAPAMBANA NA WAFUASI WA NASA WAKATI MTU MMOJA AKIUWAWA KWA RISASI

Maandamano yamezikumba kaunti za Siaya, Homa Bay na Migori wakati wafuasia wa muungano wa NASA wakipinga kutangazwa mshindi rais Uhuru Kenyatta.

Waandamanaji waliwasha moto barabarani wakipambana na polisi usiku wa jana pamoja na leo asubuhi.

Katika kaunti ya Siaya mwili wa mtu aliyepigwa risasi na polisi wakati wa ghasia hizo ulikuwa bado umelala barabarani leo asubuhi.

Baadhi ya barabara zilikuwa bado zimefungwa mapema leo asubuhi baada ya maandamano hayo ya jana usiku.

No comments

Powered by Blogger.