ATAKAYESHINDA URAIS TFF KUAPISHWA LEO HII, HAINA KUREMBA

Mgombea ambaye atashinda katika nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) anatarajiwa kuapishwa muda mfupi baad aya matokeo kutangazwa leo Jumamosi mkoani Dodoma.
Uchaguzi Mkuu wa TFF unafanyika kwenye Ukumbi wa St Gasper kwa ajili ya kuwapata washindi wa nafasi ya urais, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya mckahato wa kupiga kura kuanza.
Mwakyembe amesema rais na wajumbe watakaopatikana wataapishwa mbele ya wapiga kura wote wa uchaguzi tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakishahau haki ya waliowachagua kwa kuwaapisha nje ya utaratibu.
Uchaguzi huo unasimamiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocatus Kuuli unafanyika baada ya Jamal Malinzi kuelekea kumaliza kipindi chake cha uongozi cha miaka minne.

No comments

Powered by Blogger.