Kilichoendelea Leo Mahakamani Baada ya Jamali Malinzi Kufikishwa Mahakamani

Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itoe maelekezo mahususi kwa upande Serikali kuharakisha upelelezi, kinyume na hapo Mahakama iwasikilize na iwaachiwe.

Wakili wa utetezi, Domician Rwegoshora amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilfred Mashauri kwamba wanautaka upande wa mashtaka uharakishe upelelezi kwa sababu kesi hiyo haina dhamana, hivyo washtakiwa wakiendelea kukaa ndani wanateseka.

"Mahakama itoe maelezo mahususi kwa upande wa mashtaka kwa muda mfupi, au washtakiwa wasikilizwe ikiwezekana Mahakama iwaachie.”  Amesema Wakili  Domician Rwegoshora.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Serikali, Vitalis akaeleza kuwa upelelezi upo katika hatua ya mwisho na muda si mrefu itaanza kusikilizwa.

Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi September 9, 2017 huku akiutaka upande wa Serikali kuharakisha na ikiwezekana katika tarehe hiyo watoe taarifa kuhusu upelelezi.

No comments

Powered by Blogger.