Kesi ya Halima Mdee yasogezwa mbele mpaka Novemba 12
Kesi ya Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CHADEMA, Halima Mdee imehairishwa mpaka Novemba 12 mwaka huu itakaposomwa tena kutokana na upelelezi kutokamilika.Uamuzi huo umetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Jijini Dar es Salaam ambako Mhe. Mdee ndipo alipofunguliwa mashtaka yake yanayomkabiri ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.
Halima Mdee alikamatwa na jeshi la polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi na kukaa rumande kwa takribani siku 5 na ilipofika Julai 10 mwaka huu aliweza kupandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kusomewa mashataka yake yanayomkabiri japo alipata dhamana dhidi ya kesi hiyo kwa kusaini hundi ya Milioni 10 na wadhamini wawili.
Post a Comment