GRACE MUGABE AREJEA ZIMBABWE KIMYA KIMYA BAADA YA KUKUMBWA NA TUHUMA ZA KUMERUHI MTU AFRIKA KUSINI

Mke wa rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe amerejea nchini Zimbabwe akitokea Afrika Kusini licha ya tuhuma za kumdhuru mwanamke mmoja kwenye hoteli Jijini Johannerburg.

Grace Mugabe mwenye umri wa miaka 52, amewasili Jijini Harare mapema leo kwa mujibu wa radio moja ya Zimbabwe, licha ya kuwepo kwa jitihada za kumzuia Afrika Kusini.

Grace alikuwa anapaswa kuhudhuria mkutano siku ya jumamosi nchini Afrika Kusini lakini hakutokeza. Pia inadaiwa aliomba kupatiwa kinga ya Kidiplomasia.

Mama Mugabe anatuhumiwa kumpiga kwa waya wa umeme mwanamke mmoja mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20 kichwani na kumjeruhi.
Mwanamitindo Gabriella Engels akiwa na plasta kichwani katika eneo aliloumia baada ya kupigwa na Grace Mugabe

No comments

Powered by Blogger.