"Wangekiri makosa wakajiuzulu" - Julius Mtatiro

                                                                                      Julius Mtatiro

Mwenyekiti Kamati ya muda ya uongozi wa CUF, Julius Mtatiro ameonyeshwa kushangazwa na kitendo cha serikali kuwatuhumu wapinzani kashfa ya kushikiliza mali za Tanzania, na kusema kuwa kama kungekuwa na utu yasingefika yalipo sasa.
Kwenye ukurasa wake wa facebook Julius Mtatiro ameandika akisema kuwa pesa ambayo Tanzania inaenda kupoteza ni nyingi hivyo haina budi wahusika wawajibike, lakini badala yake wamekuwa na kiburi na kutoomba radhi.
“Bilioni 90 ni pesa nyingi sana, lakini zinakwenda kupotea hivi hivi, na wanao husika na kiburi kilichopelekea hasara hii siyo tu kwamba wamekataa kujiuzulu au kuomba radhi, bali wanatumia nguvu kubwa zaidi kutaka umma uamini kuwa wao ni watakatifu na hawafanyi makosa makubwa kama haya”, aliandika Mtatito.
Mtatiro aliendelea kuandika ….”Tungekuwa na watu wenye utu wangelitoka hadharani, wangekiri makosa yao, wakajiuzulu na kuomba wasishtakiwe. Kinyume chake, waliotutia hasara hii ndo wako mstari wa mbele kuwatisha waliofichua kashfa hii”, aliandika Julius Mtatiro.
Mtatiro pia aliendelea kuandika kwamba kama serikali ingekuwa makini, isingepoteza pesa hizo na badala yake wangeweza kuzitumia kwenye shughuli za maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi wake.
“Yani tunakwenda kuwalipa watu bilioni 90 za bure! bilioni 90 ni sawa na magari 3,000 ya wagonjwa na yangeliweza kugawiwa kila kata ya Tanzania, ni sawa na matrekta 1,500 ya kisasa na tungeliweza kuyagawa kwa nusu ya kata za Tanzania na kwa miaka mitano idadi ya makumi elfu ya wakulima wangefaidika”, aliamdika Mtatiro.  
Chanzo: eatv.tv

No comments

Powered by Blogger.