BONDIA MKONGWE WLADMIR KLISTCHO ATANGAZA KUSTAAFU NDONDI

Wakati wapenda ndondi wakisubiri kwa hamu kuona mpambano kati ya Wladmir Klistcho na Athony Joshua habari ni kuwa Wladmir Klistcho ameamua kutangaza kustaafu mchezo wa masumbwi.
Klistcho, 41, ameamua kuachana na mchezo huo aliodumu nao kwa miaka 21 na hivyo kusimamisha ndoto za wapenda masumbwi kumuona akipigana tena na Joshua.
“Nimeshashinda kila kitu ambacho nilitamani kushinda na sasa ni muda wangu kuanza kufanya mambo mengine, sikuwahi kuwaza kama nitakuwa bondia kwa muda mrefu hivi na mafanikio” alisema Wladmir.
Klistcho maarufu kama Dr Steelhammer ameshacheza mapambano 69 hadi hivi sasa, akishinda 64 na kati ya hayo alishinda 53 kwa KO na kupoteza mapambano 5.
Klistcho ameshawahi kushinda mataji makubwa ya masumbwi duniani ikiwemo IBF,WBO,WBA na IBO na taji lake kubwa la kwanza alilishindwa mwaka 1992 baada ya kumtwanga  Marcus Mclntyre.
Pambano lake kubwa la mwisho lilikuwa mwezi April pale Wembley zidi ya Anthony Joshua katika mpambano ambao Klistcho alipigwa katika raundi ya 11, na mazungumzo ya kurudia pambano hilo yalikuwa yakiendelea lakini sasa inaonekana hayapo tena.
Wladmir ni mdogo wa Vitali Klistcho ambaye naye alikuwa bondia lakini kwa sasa ni mwanasiasa nchini Ukaraine katika jiji wanalotokea la Kiev na inasemekana Wladmir naye anataka kuingia kwenye siasa kama alivyo kaka yake.

No comments

Powered by Blogger.