Wazee wa Yanga SC, watoa baraka kwa Msuva
Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Yanga, Simon Msuva
Mara baada ya kiungo wa Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania, Simon Msuva kupata nafasi ya kwenda kuanza maisha mapya ya soka la kulipwa nchini Morocco hatimaye wazee wa klabu hiyo wametoa baraka zao.
Uongozi wa baraza la wazee wa klabu ya Yanga umesema unamtakia mafanikio mema kiungo mshambuliaji wao, Simon Msuva anayetarajia kujiunga na Klabu ya Difaa El Jadidi inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

Katika mahojiano yake ya mwisho, Simon Msuva amesema
“Kila kitu kipo tayari nasubiria viza tu itoke, Ntaelekea Morroco kujiunga na klabu ya Difaa Al Jadida (washindi wa pili ligi kuu Morroco). Naondoka Yanga SC, timu iliyonilea na kunipa mafanikio”.
Msuva ameongeza kwa kusema “siondoki kwa ubaya ndio maana nimefuata taratibu zote ambapo viongozi wote wa pande mbili wameafikiana na kufanya biashara, naamini ipo siku ntarudi kuitumikia Yanga tena ila mpaka nitimize malengo yangu ya kucheza soka la kulipwa Ulaya na kuwa miongoni mwa wanasoka waliofanikiwa nchini”.Alisema Msuva.
Post a Comment