Ukaguzi wa polisi nyumbani kwa Lissu

                                           
                                                  Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu

Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ambaye alikamatwa na polisi, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akiwa anaelekea nchini Rwanda na kulala rumande leo amekwenda kupekuliwa nyumbani kwakwe.
Afisa Habari wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha kiongozi huyo kuchukuliwa na polisi na kwenda nyumbani kwake kusachiwa lakini anadai mpaka sasa haijafahamika polisi wanakwenda kufanya upekuzi wa kitu gani.  
"Polisi wamemchukua Mhe. Tundu Lissu kutoka kituo kikuu cha polisi na muda huu wanakwenda naye nyumbani kwake kwa ajili ya kupekuliwa. Hadi muda huu inapotolewa taarifa hii haujajulikana upekuzi huo unahusu kitu gani. Polisi Dar es Salaam hadi sasa hawajafafanua tuhuma za uchochezi ambazo wanadai anakabiliwa nazo, zinahusu kuchochea nini na kuwachochea akina nani, kwa ajili ya nini" alisema Tumaini Makene 
Aidha Afisa habari huyo amedai kuwa jeshi la polisi pia bado halijasema kuhusu hatima ya Tundu Lissu kufikishwa mahakamani au kuachiwa huru hivyo bado anashikiliwa na vyombo vya dola mpaka sasa. 
Tundu Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS) alifanya mkutano siku ya Jumatatu wiki hii ambapo alizungumza mambo mengi ikiwepo kuzungumzia utawala wa awamu ya tano na kulaani vitendo vinavyofanywa na polisi kuwakamata wanachama wa CHADEMA na upinzani kiujumla.

No comments

Powered by Blogger.