UGANDA YAMPIGA MTU 5-1, TAIFA STARS YAONDOLEWA MICHUANO YA AFRIKA

                                                     Uganda vs Sudan Kusini.

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeondolewa katika mbio za kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji Wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN) baada ya kutoka suluhu dhidi ya Rwanda.

Taifa Stars imeondolewa katika mbio za kufuzu michuano hiyo kwa faida ya bao la ugenini kwa kuwa katika mchezo wa kwanza matokeo yalikuwa 1-1, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Tanzania.

Mchezo wa pili umemalizika kwa matokeo ya 0-0 na hivyo sasa Rwanda imesonga mbele katika raundi ya tatu ambapo huko itakutana na Uganda.
Uganda imefika hatua hiyo baada ya kuifunga Sudan Kusini kwa mabao 5-1, baada ya matokeo ya 0-0 katika mchezo wa awali.

Mabao ya Uganda katika mchezo huo yamefungwa na Derrick Nsibambi aliyefunga mabao manne na Paul Mucureezi.

No comments

Powered by Blogger.