Sekondari 12 zajitokeza Kushiriki Mashindano ya Mdahalo katika Tamasha la Majimaji Selebuka

Mkuu wa Wilaya ya Songea,  Pololet Mgema ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mdahalo kwa shule za sekondari katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2017 akizungumza katika ufunguzi wa mdahalo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Songea,jana
Mchuano wa mdahalo kwa shule za sekondari ukiendelea. Jumla ya shule 12zikiongozwa na bingwa mtetezi, Shule ya Sekondari ya De Paul na fainali itakuwa Leo Ijumaa, 
Mchora vibonzo maarufu nchini na balozi wa Tamasha la Majimaji Selebuka Tanzania, Nathan Mpangala akizungumza na wanafunzi wa shule zilizoshiriki mdahalo kwa shule za sekondari juu ya umuhimu wa uchoraji unaoelezea changamoto na fursa zilizopo nchini kupitia Jukwaa la Mtu Kwao.
Mteja akipata msaada katika mambo yote yahusuyo masuala ya kipolisi katika banda la polisi Ruvuma ambao ni moja ya vikundi vya maonyesho katika Tamasha la Majimaji Selebuka linaloendelea mjini Songea.
Baadhi ya watu waliofanikiwa kwenda kwenye vivutio vya utalii wa ndani, katika kilele cha mlima Matogoro uliopo manispaa ya songea

Na Mwandishi Wetu Songea.
Jumla ya shule za sekondari 12 zimejitokeza kushiriki mashindano ya mdahalo kwa shule za sekondari katika Tamasha la Majimaji Selebuka linaloendelea mjini Songea,Ruvuma.
Mkuu wa wilaya ya songea, Pololet Mgema ndiye alikuwa mgeni rasmi ambapo kupitia mada ya mdahalo isemayo 'ULIPAJI KODI HAUEPUKIKI KWA TIJA YA MAENDELEO YA NCHI YETU' amehimiza suala la ulipaji kodi na kuwataka wananchi kudai lisiti kwa kila bidhaa watakayonunua.
Mdahalo huo ukiongozwa na hizo bingwa mtetezi shule ya sekondari ya De Paul, fainali itakuwa Leo Ijumaa Julai 28, baada ya mchujo.
Nyingine ni St Agness (Chipole), Songea Girls, Mfanyaraki, Ruvuma, Bombambili, Kigonsela, Emmanuel Nchimbi, Msamala, Mashujaa, London na Agustivo High Sec.
Aidha shule tatu zitaondoka na zawadi mbalimbali ikiwemo ya IPads zenye notice za kidato cha kwanza mpaka cha sita na kikombe.
Mdahalo huo umepewa nguvu na JICA, benki ya CRDB, Azam na TRA.

No comments

Powered by Blogger.