kumbe WCB walishamalizana na uongozi wa Saida Karoli kitambo
Sehemu ya picha zikimuonesha mwanamuziki Diamond akiwa na Felician Mutakyawa.
Meneja Sallam kutoka WCB kupitia akaunti yake ya Instagram ameonyesha
baadhi ya nyaraka ambazo zimewapitia kibali cha kutumia sehumu za wimbo
‘Maria Salome’ wa Saida Karoli kwenye wimbo mpya wa Diamond, ‘Salome’.
Wimbo ‘Maria Salole’ wa Saidi Karoli ni miongoni mwa nyimbo za asili
zilizofanya vizuri miaka ya 2000 na bado unaendelea kupendwa hadi sasa.
Kupitia akaunti yake hiyo meneja huyo ameandika;
“Tunakushukuru sana uongozi wa Saida Karoli na mzee Felician
Mutakyawa kutupa haki na baraka zote kutumia wimbo wa Maria Salome.”
“Tunatambua kwamba nyimbo hii itaendelea kuwa moja ya nyimbo bora kuwahi kutoka katika nchi ya Tanzania.” Amesititiza.
Post a Comment