RAIS MAGUFULI ATOA MIL. 1 KUKARABATI DIRISHA ALILOVUNJA AKIWA FORM 2


 Rais Magufuli akimwonyesha mkewe, Mama Janeth Magufuli dirisha aliloharibu na kitanda alichokuwa akilalia wakati akisoma kidato cha pili katika Seminari ya Katoke.

Mapema leo asubuhi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametembelea Shule ya Seminari ya Mtakatifu Karoli Lwanga Katoke alikosoma elimu ya sekondari ambapo ameendesha harambee iliyofanikisha kupatikana mifuko 1,000 ya saruji na mabati 150 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa majengo ya Seminari hiyo ambapo pia ametoa Shilingi Milioni 1 kwa ajili ya kutengeneza dirisha la bweni alilolivunja wakati akiwa kidato cha pili pamoja na madirisha mengine yanayohitaji matengenezo.
                                 Rais Magufuli akisalimiana wanafunzi wa Katoke Seminary.

Dkt. Magufuli alienda shuleni hapo baada ya kuzungumza na wananchi wa Biharamulo Mkoani Kagera alipokwenda kufungua barabara ya lami ya Kagoma – Biharamulo – Lusahunga.
                                                            Akizungumza shuleni hapo.

Akizungumza na wananchi wa Biharamulo, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vyote vya mafuta nchini kufunga na kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti (Electronic Fiscal Petrol Printer).
                                                      Akitoka kukagua bweni la St. Ponsian.

 Mhe. Dkt. Magufuli ameziagiza Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhakikisha vituo vyote vya mafuta nchini vinatumia mashine hizo na kusisitiza kuwa wamiliki watakaokiuka agizo hilo vituo vyao vifungwe na kufutiwa leseni.

No comments

Powered by Blogger.