Ndoto yangu ya kucheza Europa na Everton imetimia – Wayne Rooney
Wayne Rooney
Mshmbuliaji wa klabu ya klabu ya Everton, Wayne Rooney amesema ndoto yake imetimia ya aliyokuwa akiipigania tangia zamani ya kushiriki michuano ya Europa akiwa na timu hiyo.Rooney ambaye amejiunga na Everton akitokea Manchester United amesema kwasasa anajiona kama mtu mwenye bahati kurudi kwenye klabu yake ya zamani na kushiriki Europa.
“Kitu ambacho nilikuwa natamani ni kuona ni kushiriki michuano ya Europa na nikiwa na Everton kwangu naona kama ndoto yangu iliyoishi kwa muda mrefu imetimia”,amesema Rooney kwenye mahojiano yake na Everton TV.
Klabu ya Everton ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya SportPesa ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa kufuzu Europa ambapo Alhamisi hii watavaana na klabu ya MFK Ružomberok kutoka Slovakia.
Post a Comment