KISA MJAMZITO… WAZIRI AMSIMAMISHA MGANGA MFAWIDHI
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ummy Mwalimu, amemsimamisha kazi mganga mfawidhi (Clinical Officer) wa Kituo cha Afya, Mlandizi, Mkoa wa Pwani, kutokana na kumwambia mama mjamzito, Salma Khalfan, aliyefika kujifungua akanunue dawa nje ya zahanati hiyo zenye thamani ya Shilingi 180,000.
Waziri huyo ameutaka uongozi wa zahanati hiyo kuhakikisha unampatia takwimu maalum juu ya manunuzi sahihi ya dawa zilizonunuliwa na zilizopo hadi sasa kwani kitendo cha mama mjamzito kuambiwa akanunue dawa nje ya zahanati hiyo kimemkera na amesema kesho saa nne atarudi katika zahanati hiyo ili apewe maelezo sahihi.
Aidha, Mwalimu ameamua kutumia gharama zake kumhamisha mama huyo kutoka zahanati hiyo na kumwagiza mganga mkuu wa wilaya amwandikie rufaa ya kwenda Hospitali ya Mkoa ya Tumbi.
Post a Comment