Meya wa Jiji la DSM Mwita awataka wananch kuwa wa moja bila kujali itikadi ya vyama vyao.
akizungumza na waumini wa kanisa la Tanzania Assembles Of God jana katika hafla ya uchangiaji wa ujenzi wa kanisa la kisasa lililopo Kivule Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.wapili kushoto Mwenye Shati jeupe na Tai ni Diwani wa kata ya Kivule Mollel, watatu kulia ni Mchungaji wa kanisa hilo Amosi Mbiga.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waumini wa kanisa la TAG jana.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati Mwenye suti nyeusi akishangilia kwaya iliyomaliza kutumbuiza kwenye hafla hiyo ya uchangiaji wa ujenzi wa kanisa la TAG Kivule jana. Wakwanza mwenye shati jeupe ni Diwani wa kata hiyo Mollel, wapili kushoto ni Mchungaji wa kanisa hilo Amosi Mbiga.
MSTAHIKI
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema watanzania
hawajafikia hatua ya kubaguana kwa itikadi ya vyama, Dini, Kabila
badala yake wote wanapaswa kutangaza hali ya Umoja, Upendo na Mshikamano
katika nchi yao.
Meya
Mwita alitoa kauli hiyo jijini hapa jana, wakati wa harambee ya
uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa la kisasa la Tanzania Assemblies Of God
(TAG) lililopo Kivule ,Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini hapa
ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa watanzania wanapaswa kuwa
wamoja ili nchi iendelee kuwa na amani.
Alisema
yapo mambo mbalimbali ambayo yanajitokeza ndani ya nchi ambapo kama
watanzania , kwakushirikiana na viongozi wa dini kwa pamaoja wanapaswa
kusimama na kuliombea Taifa ili kuendelea kudumisha amani iliyopo.
"
Tangu nimezaliwa sijawahi kushuhudia vita, machafuko katika nchi yetu,
kikubwa huwa naona amani iliyotawala, Upendo, na umoja , sasa nawasihi
sana ndugu zangu tuendelee kuwa wamoja tusibaguane, kwa namna yoyote ile
, ili nchi yetu iendelee kuwa na amani" alisema Meya Mwita.
"Baba
wataifa Hayati Mwalim Julius Nyerere enzi ya uhali wake alikuwa
akisisitiza sana kulinda amani ya nchi yetu, na sisi ambao tupo hai hadi
sasa , mambo ya vyama, Udini, Ukabila tuweke pembeni tusimame kama
Taifa moja.
Awali akijibu
risala iliyoandaliwa na uongozi wa kanisa hilo, Meya Mwita aliahidi
kuchangia katika ujenzi huo mifuko 100 ya Simenti na kiasi cha Fedha
shilingi 500,000 huku aliwataka waumini wa kanisa hilo kujitolea ili
kufanikisha ujenzi huo.
Risala
hiyo ilieleza kujenga kanisa la kisasa lenye uwezo wa kuchukua waumini
600 ambapo jumla ya shilingi milioni 95 zinahitajika ili kukamilisha
ujenzi huo.
Post a Comment