JOHN BOCCO ATUA AFRIKA KUSINI, NI BAADA YA MBARAKA YUSUPH KUWA MAJERUHI

Mshambuliaji mpya wa Simba, John Raphael Bocco ametua nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichopo nchini humo kutokana na mchezaji Mbaraka Yusuph kuwa majeruhi.
Taifa Stars inashiriki michuano ya COSAFA ikiwa ni nchi mwalikwa lakini hadi sasa imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya jana kuifunga Bafana Bafana bao 1-0 katika Robo Fainali.
Ofisa Habari wa Shirikishop la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amethibitisha juu ya safari hiyo ya Bocco kwa kusema anaenda kuchukua nafasi ya Mbaraka ambaye ni majeruhi.
Pamoja na taarifa hizo inaelezwa kuwa Bocco ameitwa kwa ajili ya mechi ya kwanza ya kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Rwanda Julai 14 mjini Mwanza, kwa kuwa kwa sasa hataweza kuingizwa kwenye COSAFA.
Tanzania sasa itacheza dhidi ya Zambia, keshokutwa  Jumatano katika Nusu Fainali, wakati Afrika Kusini wanaangukia kwenye michuano ya Plate, inayohusisha timu zilizotolewa hatua ya Robo Fainali.

No comments

Powered by Blogger.