BRAZUKA KIBENKI: Maofisa wa benki kuonyeshana kazi viwanjani

                     Martin Komba wa DTB (kulia) akimtoka Hezbo wa NMB katika pambano la jana

MSIMU wa tatu wa michuano ya BRAZUKA KIBENKI unaoshirikisha taasisi za kibenki katika michezo ya mpira wa miguu na kikapu unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam.

Katika msimu huu michuano hiyo itashirikisha timu 15 ambazo ni NMB (Mabingwa watetezi), DTB, Barclay’s, BancABC, Exim, Stanbic, BOA, UBA, Letshego, EcoBank, CRDB, BOT, Azania, TPB, Access na UBA.

Mmoja wa maofisa wa benki ya Exim, Frank Rweyemamu ambaye pia ni mwanachama wa tawi la Simba Makini linalomiliki mtandao huu alivitaja viwanja vitakavyotumika kuwa ni Gymkhana na DonBosco.
“Michuano ya mwaka huu itafanyika katika viwanja vya Gymkhana kwa mpira wa miguu huku mechi za mpira wa kikapu zikitarajiwa kuchezwa katika uwanja wa DonBosco.” Alisema Rweyemamu.


Jana kulikuwa na mchezo wa ngao ya hisani ambapo mabingwa watetezi NMB walikubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa DTB katika mchezo wa kuashiria kuanza kwa michuano hiyo.

Bingwa wa msimu huu atakabidhiwa kikombe pamoja na medali.

No comments

Powered by Blogger.