Shilole Ataja Sifa za Mwanaume Anayemtaka
Zuwena
Mohamed ' Shilole' anayetamba na hit ya 'hatutoi kiki' amefunguka na
kudai kwamba haitaji kuolewa na mwanaume mwenye pesa kwani wengi wao
hutumia mali zao kama fimbo ya kuwachapa na kunyanyasia wanawake zao.
Akiwa
Kikaangoni kwenye ukurasa wa Facebook wa EATV, Shilole amefunguka kuwa
yupo tayari kuolewa lakini mpaka atakapo pata mwanaume atakayekidhi
vigezo vyake huku akitaja pesa siyo kitu anachokitanguliza bali heshima,
upole na ukarimu.
"Natamani
sana kuolewa lakini mpaka nimpate mtu mwenye vigezo ninavyohitaji mimi,
napenda mwanaume anayejali, atakayeniheshimu lakini awe pia anafanya
kazi kama hafanyi kazi simtaki. Lakini pia wanaume wenye pesa siwataki
maana tunawaona huko majumbani wanavyotumia kama fimbo kuwanyanyasa wake
zao" Shilole alifunguka.
"Mimi
siangalii sana muonekano kwani unaweza kutengenezwa lakini ukiwa mfupi
mimi sitakukubali nahitaji mwanaume mrefu na mwenye heshima na
anayejituma kwenye utafutaji" aliongeza Shilole.
Post a Comment