Nape Nnauye afunguka kuhusu ukimya wa Kinana, Mwenendo wa shughuli za Bunge pamoja Polisi Kutumia Nguvu Kubwa
Na Regina Mkonde
Mbunge
wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amefunguka kuhusu masuala mbalimbali
ikiwemo, ukimya wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, muenendo wa
shughuli za Bunge pamoja na tukio lililotokea hivi karibuni la Askari
Polisi mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kufyatua risasi hewani
mbele ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima baada ya kutokea
majibizano yaliyosababishwa na dereva wa Malima kuegesha gari vibaya.
Nape
amefunguka hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na
wanahabari ambapo alisema, Kinana ambaye baadhi ya watu wanadai kuwa
ukimya wake umetokana na kujiuzulu, yuko katika wadhifa wake wa ukatibu
mkuu na anaendelea kufanya kazi za chama.
“Mimi
sio msemaji wa chama, lakini Katibu Mkuu yupo na anafanya kazi yake
kama kawaida…., mimi bado ni mwanachama na muumini mzuri wa CCM
inayopenda haki, na nina amini hiki ndicho chama pekee bora
kitakachoweza kuwakomboa watanzania pamoja na kuamiwa ikiwa kitatekeleza
mkataba wake na wananchi ambao ni wa kutimiza ahadi zake ilizo
ziahidi,” alisema.
Kuhusu
tukio la Askari Polisi kufyatua risasi hewani, ambalo Kamishna wa Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro alisema
ulikuwa uamuzi wa busara wa kuondoa taharuki katika tukio hilo, na mbinu
ya kuwatia nguvuni watuhumiwa.
Nape
alishauri vyombo vya dola kutotumia nguvu kwani kitendo hicho kitajenga
hofu na chuki baina ya serikali na wananchi na hata kwa chama tawala
CCM, huku akiisihi serikali kuondoa vitendo vinavyotia hofu wananchi.
“Ni
vizuri vyombo vya dola vikatimiza majukumu yake kwa kuwa ni vyombo vya
wananchi, si vizuri vikitumia nguvu kubwa pale isipostahili. Ifikie
hatua raia asiye na silaha Polisi wasitumie nguvu kushughulika naye kwa
kutumia silaha. Nimeona ile video ikionyesha Malima alikuwa anauliza
chanzo cha tatizo,” alisema na kuongeza.
“Kuna
nchi tamaduni zake ni kutumia mabavu na nyingine zinatumia demokrasia,
nchi yetu utamaduni wake si wa kutumia nguvu, tumezoea kuelewana kwa
mazungumzo. Vyombo vya dola visitumie nguvu kwa kuwa tunajenga usugu
usio na maana. Na kama kuna mazingira hatarishi basi nguvu itumike.”
Kuhusu
mienendo ya shughuli za Wabunge Bungeni, aliwataka wabunge kutekeleza
majukumu yao ikiwemo kuwawakilisha na kusimamia vema masilahi ya
wananchi wanaowawakilisha, pamoja na kuisimamia serikali kutekeleza
vizuri majukumu yake.
“Bunge
ni mkutano wa wananchi, na wabunge wapo kwa niaba ya wananchi katika
kupitisha na kushauri mipango ya serikali. Ni vizuri wasimame katika
maeneo yao, wasiwe wapiga makofi, pale serikali inapofanya vizuri
ipongezwe na inapofanya vibaya ikosolewe,” alisema.
Kuhusu
Uhuru wa Vyombo vya Habari, alisema ifikie hatua wananasiasa wawe na
ngozi ngumu ya kuvumilia kukosolewa na watu kupitia vyombo vya habari.
Pia ameshauri wananchi wanaotaka maonesho ya vikao vya bunge moja kwa
moja, kuuomba mhimili huo kubadilisha sheria zake ambazo zimeipa mamlaka
ya kuamua namna ya kuendesha shughuli zake.
“Naamini
uamuzi wa siku ile wa kuzuia shughuli za bunge live ulikuwa sahihi
sababu sheria zinasema Bunge litaendeshwa kwa sheria zake. Wananchi
wanaozungumzia Bunge live, waliombe libadilishe sheria zake ili lianze
kuonyeshwa live,” alisema
Post a Comment