Simba SC kufukuza wachezaji wake tano wa kigeni
Wanamsimbazi na hata baadhi ya viongozi mpaka sasa hawaamini kama timu yao ndio imeukosa ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara msimu huu, lakini moja ya wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa klabu hiyo, Hamis Kilomoni amefichua siri nzito kuwa kuna wachezaji watano wa kigeni watatemwa na klabu hiyo.
Kilomoni amesema kuna wachezaji watano wa kigeni watatemwa klabuni
hapo ili kupisha wazawa kuipigania klabu hiyo kwani wanagharama ndogo na
wanajitoa kuipigania timu kwa jasho na damu.
Kilomoni aliyewahi kuwa mchezaji na kiongozi wa Simba kabla ya
kuwa Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini, alisema Simba haikupata huduma
sahihi kwa nyota wake saba wa kigeni iliowasajili msimu huu kwa uwezo
mdogo walionao, hivyo anaona ni bora idadi yao ipunguzwe ibaki wawili
tu.
Alisema mabosi wa Simba walifanya kosa kubwa kuwadharau wachezaji
wazawa na kuwakimbilia wageni ambao wamekuwa hawana msaada wowote zaidi
ya kuitia gharama kubwa ya kuwahudumia.
Timu ya simba
“Tulikuwa na wachezaji wengi kutoka kikosi B, lakini sijui nini kilitokea wakatolewa, huko waliko wanafanya vyema na hata kuisumbua Simba, halafu sisi tukakimbilia wageni saba ambao ukiniuliza faida yake hata sijaiona, nafikiri tunapaswa kuangalia upya hili suala la wachezaji wa kigeni halisaidii soka letu, Simba kama kuna wachezaji wa kigeni wanaostahili kubaki na walioisaidia timu wako wawili tu hawa wengine sioni wanachokifanya.” Alisema Kilomoni.
Hata hivyo Kilomoni hajawataja nyota wanaostahili kusalia, japo Simba
kwa sasa ina wachezaji wa kigeni ambao ni Method Mwanjali, Juuko
Murshid, Fredrick Blagnon, Janvier Bokungu, Laudit Mavugo, James Kotei
na kipa Daniel Agyei.“Tulikuwa na wachezaji wengi kutoka kikosi B, lakini sijui nini kilitokea wakatolewa, huko waliko wanafanya vyema na hata kuisumbua Simba, halafu sisi tukakimbilia wageni saba ambao ukiniuliza faida yake hata sijaiona, nafikiri tunapaswa kuangalia upya hili suala la wachezaji wa kigeni halisaidii soka letu, Simba kama kuna wachezaji wa kigeni wanaostahili kubaki na walioisaidia timu wako wawili tu hawa wengine sioni wanachokifanya.” Alisema Kilomoni.
Chanzo : Mwanaspoti
Post a Comment