Naibu waziri Tamisemi,Seleman Jafo anusurika kifo ajalini Mbeya

 Gari la Naibu Waziri wa Tamisemi likionekana baada ya kugongwa katika ajali hiyo.
                           Gari lililoigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni.
            Askari wa usalama barabaran wilaya Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea.
Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amepata ajali eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ta Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari Waziri walikuwa watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na wote walitoka salama katila ajali hiyo. Alisema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanyiwa uchunguzi kama wameumia kwa ndan au laa! Lakin bahati nzuri Daktari aliyewafanyia
uchunguzi alisema hawakuumia popote ni wazima.
Alisema baada ya hapo Waziri na watu wengine waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge
 
 

Picha zote kwa hisani ya Mbeya yetu

No comments

Powered by Blogger.