TUTAWAONESHA SIMBA SOKA LA BARCELONA-RUVU SHOOTING

Timu ya Ruvu Shooting, imeitambia kuifunga Simba pindi timu hizo zitakapokutana keshokutwa Jumatano kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Ofisa habari wa Ruvu Shooting Massau Bwire amesema, hawana wasiwasi na mchezo huo kwani wameonekana kujipanga vizuri na wana uhakika wa kuibuka kidedea kwa kuwa kwa sasa soka lao ni kama Barcelona.Tumejipanga vizuri na ninauhakika tutaibuka washindi kwani kwa sasa timu yetu imekuwa ikicheza soka la pasi nyingi kama Barcelona kwa hiyo wao wasubiri waone tutakavyofanya uwanjani, amesema Bwire. Bwire amesema, anaamini mchezo huu utakuwa wa kiufundi zaidi kwani timu zote mbili zimeokana kuwa na wachezaji wazuri, lakini akadai kuwa mpaka mwisho wa mchezo huo wao ndio wataibuka kidedea. Naamini mpaka mchezo kumalizika mimi pamoja na timu yangu tuitaibuka kidedea kwani tumejipanga vizuri na tunajiamini kuweza kuwakabili Simba, amesema Bwire.

No comments

Powered by Blogger.