Kuna kitu kimeturudisha nyuma Yamoto Band – Aslay
Yamoto Band
Mmoja kati ya wasanii wanaounda Kundi la Yamoto Band, Aslay ambaye hivi sasa ameanza kufanya kazi peke yake nje ya kundi hilo, amefunguka kwa kudai kuwa kuna vitu nimewakwamisha na kushindwa kwenda mbele kama kundi.
Muimbaji huyo amedai kipindi cha nyuma walikuwa wanapata show nyingi sana jambo ambalo lilipelekea kuwa na uwezo wa kufanya video kubwa hata nje ya nchi lakini baadaye mambo yalibadilika na kupelekea kufanya video zao hapa hapa bongo.
“Mimi nafikiri kwamba mipango yetu tu wenyewe, kipindi kile tunatoa ile video ‘ Madoido’ kulikuwa na show nyingi zinaongozana ambazo zilituzuia kwenda kutengeneza video nyingine lakini si unajua tulikuwa tunajenga pia kwa hiyo kifupi ni kama tulijisahau na kuteleza kusema ukweli,” alisema Aslay.
Aliongeza, “Tukarudi tena tukafanya ‘Suu’ ambayo tuliifanya Zanzibar na tukawa na pesa kabisa ambayo ingetuwezesha kutengeneza video nyingine Afrika Kusini lakini hapo katikati tulifanya vitu fulani mchanganyiko ambavyo siwezi kuvisema vikaturudisha tena nyuma” alisema Aslay
Mbali na Aslay msanii mwingine kutoka kundi hilo Beka Flavour naye ametoka na wimbo wa peke yake akiwa chini ya menejimenti nyingine.

Post a Comment