Niliachana na Harmonize miezi 3 iliyopita lakini…- Wolper
Jacqueline Wolper
Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amedai aliachana na aliyekuwa mpenzi wake Harmonize miezi 3 iliyopita lakini waliamua kuficha kwaajili ya shughuli zao za kibiashara.
Muigizaji huyo ambaye alicheza vitendo kwenye video ya wimbo ‘Niambie’ wa Harmonize, amedai wakati kazi hiyo inatoka walikuwa tayari wameachana lakini waliamua kushirikiana katika promo ya wimbo huo ambao unafanya vizuri.
“Nyie mnajua sisi tumeachana juzi? Tumeacha miezi mitatu iliyopita kabla hata ya wimbo wake Niambie haujatoka,” Wolper alikiambia kipindi cha Shilawadu cha Clouds TV.
Aliongeza ,“Sisi wenyewe tuliamua kukaa kimya kwa sababu kuachana sio kugombana kuna kesho mnaweza kushirikiana katika mambo mengine ya kibiashara,”
Hata hivyo muigizaji huyo aligoma kueleza sababu ya kuachana na muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Happy Birthday’.

Post a Comment