MEYA MWITA: AKINA MAMA NDIYO NGUZO YA TAIFA
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye kofia katikati akizungumza na wakina mama (hawapo pchani)
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye kofia katikati akizungumza jambo na Mwanaharakati wa kipindi cha Wanawake Live Joyce Kiria wa kwanza kulia , wakati wa ufunguzi wa semina ya vikundi vya wakina mama vya wanawake Live iliyofanyika Pugu jijini hapa leo.kushoto ni Diwani wa kata ya Pugu Henry Kilewo.
Wakimama waliohudhuria semina hiyo wakimshangilia Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita (hayupo pichani) kutoka kushoto ni Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwa kwenye picha ya pamoja na joyce kiria na Diwani wa kata ya Pugu Henry Kilewo.
NA CATHERINE ALLAN/bintitz.blog
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema anatambua mchango mkubwa unaotokana na akina mama na hivyo kuwataka wanaume kuwaunga mkono kwaasilimia 100 katika shughuli za maendeleo.
Meya Mwita alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa vikundi vya akina mama vya Wanawake Live uliyofanyika Pugu, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Meya Mwita alisema wakina mama ndio msingi mkubwa ndani ya familia ,Taifa kutokana na mchango ambao huutoa jambo ambalo linaleta ustawi mkubwa wa maendeleo.
Aliongeza kuwa licha ya changamoto ambazo hukutana nazo lakini wamekuwa ni watu wasio kata tamaa hivyo akasisitiza kuwa wakina baba wanatakiwa kutoa ushirikiano wao kwa asilimia 100.
Aidha Meya Mwita aliwapongeza wa kina mama kutokana na ubunifu waliokuwa nao kila kukicha katika kujitafutia maendeleo na hivyo kuwa msaada mkubwa ndani ya familia zao ikiwemo kuwasaidia majukumu wakina baba.
“
Natambua mchango wenu sana, mmekuwa wabunifu , mnajishughulisha kwenye mambo
mbalimbali ya kimaendeleo, mmekuwa mstari wa mbele kutengeneza miradi ambayo inasaidia
kwenye familia zenu bila hata wakina baba kushiriki.
“
Hivi sasa mmeanzisha vikoba hii yote ni katika kujituma kwenu ili muondokane na
umasikini, nawapongeza sana” alisema Meya Mwita.
Akizunguzungumzia changamoto zilizopo
kwenye dampo, la Pugu Kinyamwezi, Meya Mwita alisema wameanza kuandaa utaratibu
ambao utawasaidia kuondokana na chagamoto hizo.
Alisema suala la dampo limekuwa ni changamoto
kubwa lakini hadi kufikia Agosti mwaka huu, utaratibu huo utakuwa umeshatolewa.
Akizungumzia suala la maji ,alisema kuwa
Kata yaPugu imekuwa na changamoto hiyo na hivyo kuwa kero kwa wakina mama
lakini kwa sasa upo mpango wakuwawezesha kupata visima vitatu vya maji.
Alisema kwenye shughuli za maendeleo
hakuna mambo ya vyama na kwamba viongozi walipo kwenye nafasi zao wanatakiwa kuwatumikia
wananchi wote ili kuhakikisha wanapata maendeleo waliyoahidiwa.
“ Kwenye maendeleo hakuna
mambo ya vyama, kila mmoja anahitaji maendeleo, mambo ya vyama hivi sasa tunayaweka
kando, ili kupata muda wa kufanyakazi moja tu, ya kuwatumikia wananchi ambao
mmetuchagua” alisistiza.
“ Ndani ya jiji hili tunataka kuleta
maendeleo, ili mwaka kesho nikija kusimama hapa yale ambayo tunayazungumza leo,
tusiyarudie tena na badala yake tuzungumze mambo mengine.
Post a Comment