Maxime: Nitatua Kuinoa Yanga SC Msimu Ujao
Said Ally | CHAMPIONI | Dar es Salaam
KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amefunguka kuwa anaweza kutimkia na kujiunga na Yanga kutokana na kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina raia wa Zambia kuukubali uwezo wake huku akitaka kufanya naye kazi.
Maxime amekuwa na mafaniko makubwa ndani ya msimu huu baada ya kuisaidia Kagera Sugar kumaliza katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi wakimaliza na pointi 53.
Yanga na Kagera walikutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar ambapo Maxime alishuhudia kikosi chake kikifungwa kwa mabao 2-1.
Kocha huyo ameliambia Championi Ijumaa, kuwa atatua Yanga endapo wakimalizana na viongozi wa timu hiyo kwani licha ya Lwandamina kumhitaji ndani ya benchi lake lakini kwa upande wake yupo tayari kufundisha sehemu yoyote.
“Baada ya mechi yetu na Yanga ya msimu uliopita dhidi ya Yanga, kocha wao, Lwandamina alichukua mawasiliano yangu ambapo baadaye tulikutana na kuzungumza juu ya mambo mbalimbali lakini kubwa ni namna ya kujiunga na timu yao kwani anataka kufanya kazi na mimi.
“Licha ya kuongea huko, lakini mimi ni kocha siwezi kusema kwamba nitajiunga na timu fulani, lolote linaweza kutokea endapo tu tutakubaliana kwa vitu ambavyo nitakuwa navihitaji kwani huko nyuma nilishatoka Mtibwa na kwenda Kagera na hakutakuwa na maajabu kutoka hapa na kutua ndani ya timu hiyo,”alisema Maxime.

Post a Comment