MASHINDANO YA MCHEZO WA DRAFT YA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM YAMALIZIKA, NAIBU MEYA TEMEKE AMPONGEZA

 Naibu Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Temeke , ambaye pia ni Diwani wa kata ya Temeke,   Feysal Salum , akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa fainali hizo za michuano ya Draft Mkoa wa Dar es salaam zilizofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.
 Naibu meya wa Halmshauri ya Manispaa ya Temeke, mbaye pia ni  Diwani wa kata ya Temeke,  Feysal, (mwenye shati damu ya mzee) akifuatilia kwa makini fainali za michuano ya mchezo wa Draft Mkoa wa Dar es salaam, zilizofanyika jana viwanja vya Mwembe Yanga Wilayani Temeke Jijini Dar es salaam .
 Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala , ambaye pia ni Diwani wa kata ya Temeke,  Feysal Salum, akizungumza na waandishi wa habari mara kwa niaba ya ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam  Isaya Mwita baada ya kumalizika kwa fainali hizo za michuano ya Drafti Mkoa wa Dar es salaam zilizofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Jijini Dar es salaam.
 Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,  ambaye pia ni Diwani wa kata ya Temeke Feysal  Salum,  akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa michuano hiyo,katika mashindano hayo  mshindi wa kwanza alipata zawadi ya pesa taslim sh.200000/, , wapili 100, 000 na watatu 50,000.
Mratibu wa mashindano ya fainali ya michuano ya mchezo wa Drafti Mkoa wa Dar es salaam, (Draft Compitition) Jamali Deogratus, akizungumza na waandishi wa habari kabla ya fainali hizo kufanyika huku akitoa maelekezo pamoja na faida za mchezo huo kwa jamii na wadau mbalimbali wa mchezo wa Draft hapa nchini.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, ambaye pia nia Diwani wa kata ya Temeke Feysal  Salum,  akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mchezo huo.


MASHINDANO ya mchezo wa Draft ya Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaa Isaya Mwita yamemalizika jana na kufungwa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Feysal Salum  ambapo jumla ya washindi wa tatu waliibuka kidedea na kujinyakulia zawadi kila mmoja.
Mashindano hayo ambayo yalianza Mei 13 na kufunguliwa na Meya Mwita yalikuwa na jumla ya washiriki 64, yalifikia tamati hiyo jana ambapo mshindi wa kwanza Kiraba Ngibombi ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Draft mkoa wa Dar es Salaam alipata pesa taslimu 
sh.200, 000.
Aidha mshindi wa pili katika mashindano hayo ni William Mgata , maarufu kama Bad Face ambaye alijinyakulia kitita cha sh.100,000 na mshindi wa tatu alikuwa ni Hossein Ally aliyepata zawadi ya sh.50,000.
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Jiji, Naibu Meya wa Temeke ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM ,  Feysal pamoja na mambo mengine alimpongeza Meya Mwita kwakuanzisha mashindano hayo na kuahidi kumuunga mkono.
Naibu Meya Feysal alisema kwamba kutokana na umuhimu aliouonyesha mstahiki Meya wa jiji, atashirikiana nae ili kuwa walezi wa chama hicho na hivyo kuwawezesha kwenye mchezo huo.
“ Nampongeza Mstahiki Meya wa jiji kwa kuliona hili jambo, pia kutoa heshima kubwa kulifanya ndani ya kata yangu, amefanya jambo zuri sana, sasa kwa umuhimu huo nipo tayari kumuunga mkono, nitashirikiana naye ili kuwa walezi wa chama hiki” alisema Naibu Feysal.
 Aliongeza kuwa,” nataka ifikie mahala, muwe mnaenda kushindana hata mikoani, jambo ambalo kwakushirkina na Mstahiki Meya wa jiji Mwita, Mbunge wa jimbo hili Abdala Mtolea, tutawadhamini , muda wowote ambao mtahitaji nyie” alisisitiza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mchezo huo ambaye ndie aliibuka mshindi wa kwanza Kiraba, alisema kuwa alichokifanya Mstahiki Meya wa jiji ni kufungua njia ya mchezo huo na hivyo kusisitiza kwamba kufanyika kwa usajili wa chama hicho.

“ Tunampongeza sana Meya wa jiji kwa kuweza kufanikisha jambo hili, limeonyesha msisimko mkubwa, watu wengi wamejitokeza, hii ni heshma kwake,  kwenye mengine kutakuwa na hamasa kubwa zaidi kutokana na hili lililofanyika leo” alisema Kiraba.
Mashindano ya mchezo wa Draft yalidhaminiwa na Mstahiki Meya wa jiji Mwita , ikiwa na lengo la kuhamasisha michezo mingine iweze kufahamika kama ilivyo kwenye mpira wa miguu na michezo mingine.

No comments

Powered by Blogger.