MISRI YATINGA FAINALI AFCON KWA MATUTA

Misri imefikisha rekodi ya kutinga mara tisa katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, ikiwafunga Burkina Faso magoli 4-3 kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya kutoka sare ya goli 1-1 na Burkina Faso.

Kipa mkongwe Essam El Hadary amedhihirisha kuwa ni shujaa wa Misri, kwa kuokoa penati iliyopigwa na Bertrand Traore na kuisaidia kupata ushindi.

Katika dakika za kawaida za mchezo huo Mohamed Salah aliifungia Misri goli la kwanza kwa shuti zuri la kuzungushwa lakini Burkina Faso wakasawazisha kupitia kwa Aristide Bance.
             Essam El Hadary akipangua mkwaju wa penati ya Bertrand Traore
  Bertrand Traore akionekana mwenye mawazo baada ya kukosa penati

No comments

Powered by Blogger.