Mama Akutana na Mwanaye Aliyepotea Zaidi ya Mwaka Kupitia Video ya Wanandoto ya Kala Jeremiah
Kala Jeremiah akiwa katika pozi na Adam siku ya kuandaa video ya wimbo wa Wanandoto.
MAMA wa mtoto mmoja aitwaye Adam
mwenye umri wa miaka 14, amefanikiwa kukutana na kijana wake huyo baada
ya kupotezana naye kwa zaidi ya mwaka mmoja na hatimaye kumuona kwenye video ya wimbo wa mwanamuziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah uitwao WANANDOTO.
Akiongea na tovuti hii, Kala anasema;
“Siku tatu zilizopita nilipigiwa simu na mtu mmoja akaniambia kuna mama kamuona mtoto wake kwenye video yangu ya Wanandoto na mtoto huyo alipotea tangu mwaka jana mwezi wa tisa, mama wa mtoto alifanya jitihada zote za kumpata mtoto wake bila
mafanikio.
mafanikio.
“Juzi juzi mama huyo akiwa anatazama
video ya WANANDOTO akamuona mwanaye huyo hali iliyopelekea kupata
mshangao na mshituko ndipo alipoamua kumtafuta mtangazaji fulani wa
redio ambapo mtangazaji huyo alinitafuta na kuniunganisha na mama huyo.”
Baada ya kukutana na mama Adam, Kala
anasema mama alimueleza kwa masikitiko makubwa jinsi mtoto wake
alivyopotea tangu Septemba mwaka jana na alimtafuta sana kila sehemu,
kwa waganga wengi alienda, kwenye maombi ya kila aina lakini
hakufanikiwa kumpata mwanaye mpaka alipokuja kumuona kwenye video ya
Wanandoto.
Kala akiendelea kuchonga na tovuti hii, aliongeza;
“Baada ya mama huyo kunieleza yote hayo
nikawasiliana na kituo cha kulelea watoto cha CHAKUWAMA ambapo mtoto
Adam analelewa nikawaeleza habari hii wakakiri kweli Adam yupo na ni
kweli walimpata mwaka jana mwezi wa tisa.
“Basi nikawasiliana tena na mama yake
Adam na kumwambia kuwa nimewasiliana na mlezi wa kituo amekiri kuwepo
kwa Adam kituoni hapo na kwakuwa mimi sipo Dar kwa muda huu
nikamuunganisha mama Adam na mlezi wa kituo kile wakawasiliana na jana
mama Adam amefika kituoni pale na kuonana na mwanaye na amefurahi sana.”
Alimalizia staa huyo wa ngoma ya Wanandoto.
Video iliyopelekea mama Adam kumpata mwanaye hii hapa;
Post a Comment